News

Mafunzo  maalum yaliyolenga Uzingatiaji Sheria, Kanuni, Taratibu katika Utendaji wao wa kazi hususan katika Masuala ya Nidhamu

Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania wameshiriki Mafunzo  maalum yaliyolenga Uzingatiaji Sheria, Kanuni, Taratibu katika Utendaji wao wa kazi hususan katika Masuala ya Nidhamu na kufanyika katika Ukumbi wa TAFORI, Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia Januari 28 hadi 29 yaliandaliwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Miongoni mwa Washiriki wa Mafunzo hayo ni Mameneja wa Mikoa, Baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Uhasibu na Utawala pamoja  na Wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (TAMICO) wa Makao Makuu na Mikoa.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uendeshaji Bwana Hija Ally Malamla.