Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeeleza umuhimu wa matumizi ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence - Al na mabadiliko ya kidijitali katika kuimarisha utekelezaji wa shughuli za uhandisi, ikiwemo usimamizi wa matengenezo ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wahandisi (Annual Engineers Day 2026) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Mhandisi Joel Mwambungu, amesema maendeleo ya teknolojia yanahitaji wahandisi kuendana na mabadiliko ya kidijitali na kutumia teknolojia mpya katika kuongeza ufanisi wa shughuli za kitaalamu.
Mhandisi Mwabungu amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa kwa wahandisi kupata maarifa na ujuzi kupitia mada mbalimbali, hususan matumizi ya Al katika shughuli za uhandisi, pamoja na kuwapokea wahandisi wapya walioingia katika orodha ya Wahandisi Wataalamu (Professional Engineers) baada ya kula kiapo cha kuzingatia maadili ya taaluma.
Amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia yanapaswa kwenda sambamba na weledi na maadili ya uhandisi, ili kuhakikisha ubunifu wa kiteknolojia unatumika ipasavyo katika kuboresha huduma na usimamizi wa miundombinu.
Mhandisi Mwambungu amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa kwa wahandisi kupata maarifa na ujuzi kupitia mada mbalimbali, hususan matumizi ya Al katika shughuli za uhandisi, pamoja na kuwapokea wahandisi wapya walioingia katika orodha ya Wahandisi Wataalamu (Professiona Engineers) baada ya kula kiapo cha kuzingatia maadili va taaluma.
Amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia yanapaswa kwenda sambamba na weledi na maadili ya uhandisi, ili kuhakikisha ubunifu wa kiteknolojia unatumika ipasavyo katika kuboresha huduma na usimamizi wa miundombinu,
"Dunia sasa hivi inahitaji teknolojia, na teknolojia bila wahandisi wabobezi hatuwezi kufikia hatua tunayotaka," amesema Mhandisi Mambungu.