News

WATUMISHI TANROADS WAKUMBUSHWA HAKI NA WAJIBU WAO

WATUMISHI TANROADS WAKUMBUSHWA HAKI NA WAJIBU WAO

Dodoma, 19 Machi, 2026

Watumishi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kutoka Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma wamekumbushwa haki na wajibu wao kupitia HR Kliniki inayoendelea nchi nzima.

Akizungumza, Afisa Rasilimali Mwandamizi, Bw. Adam Chitenda, amesema kliniki hiyo imeandaliwa na Mtendaji Mkuu ili kuwapa watumishi uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, na hivyo kuongeza uwajibikaji na ufanisi kazini. Ameongeza kuwa zoezi hilo linafanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na linatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 2026.

Kwa upande wao, Afisa Rasilimali Watu Mkoa wa Dodoma, Bw. Geofrey Siao, amesema kliniki hiyo italeta tija kubwa katika utendaji;  huku Afisa Manunuzi,  Bi. Tulamwidika Mlote akieleza imewasaidia kuondoa kufanya kazi kwa mazoea na kuongeza uelewa wa maadili.

Naye Mkuu wa Idara ya Matengenezo, Mhandisi Elisony Mweladzi amesema imeongeza uelewa wa haki kama likizo na malipo ya ziada, na kusisitiza kuendelezwa kwa kliniki hizi ili kuongeza ufanisi kwa watumishi wote.