News

SERIKALI YA CHUO CHA MIPANGO NA UONGOZI WA SHULE YA MSINGI YA JENERALI MUSUGURI YATOA SHUKRANI KWA TANROADS KWA TAA ZA USALAMA

SERIKALI YA CHUO CHA MIPANGO NA UONGOZI WA SHULE YA MSINGI YA JENERALI MUSUGURI YATOA SHUKRANI KWA TANROADS KWA TAA ZA USALAMA

Dodoma, 16 Machi, 2026

Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mipango na Uongozi wa Shule ya Msingi ya Jenerali Musuguri imeishukuru Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma kwa kufunga taa za barabarani kwenye barabara kuu za Dodoma – Bereko na Gairo – Dodoma, zenye kuruhusu watembea kwa miguu kuvuka kwa usalama.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MISO), Bw. Fahad Mohamed, amesema wanafunzi walikuwa wakigongwa na magari makubwa na madogo kutokana na kutokuwepo kwa taa, na kufurahishwa na hatua hii itakayowezesha madereva kusimama pale taa nyekundu inapoashiria.

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Wanafunzi, Bw. Nicodemas Nkupama, amesisitiza wanafunzi kutumia kivuko hicho kwa uangalifu, kuangalia vyombo vinavyopita, na kuhakiki alama za taa kabla ya kuvuka.

Bi. Mose Malelo, mwanafunzi wa mwaka wa pili, amebainisha kuwa taa hizi zitasaidia kufika madarasani kwa wakati na kuondoa ucheleweshaji. Mwalimu Msaidizi Bi. Mwasiti Mohamed ameongeza kuwa taa hizi pia zitarahisisha kazi ya mlinzi wa barabara, ambaye sasa atapata fursa ya kupumzika.

Dada Mkuu Bi. Caroline Ernest na kaka mkuu Juma Magoti wameishukuru serikali ya wanafunzi na TANROADS kwa hatua hii, wakiwahimiza madereva kufuata alama za usalama na kuwa makini karibu na kivuko cha barabara.

Naye kaka mkuu wa shule hiyo, Juma Magoti ameishukuru serikali kwa kuweka taa hizo anaamini kwa kiasi kikubwa zitawasaidia kuvuka barabara hiyo kubwa kwa usalama