News

WAZIRI WA UJENZI, AMEKAGUA NA KURIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGENEZO YA BARABARA YA DODOMA - IRINGA

WAZIRI WA UJENZI, AMEKAGUA NA KURIDHISHWA NA MAENDELEO YA MATENGENEZO YA BARABARA YA DODOMA - IRINGA

Dodoma, 25 Februari, 2026

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, amekagua na kuridhishwa na Maendeleo ya matengenezo ya barabara ya Dodoma - Iringa eneo la Fufu ambalo lilikuwa likijaa maji kipindi cha mvua na kusababisha adha kwa wananchi wa eneo hilo.

Waziri Ulega amekagua eneo hilo leo tarehe 25 Februari, 2026 akiwa njiani kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ambapo amempongeza Meneja wa Wakalaya Barabara Tanzania (TANROADS), mkoani Dodoma Mhandisi Zuhura Amani kwa kukamilisha mradi huo sambamba na usimikaji wa taa 46 za barabarani. Aidha Waziri Ulega amemuelekeza Mtendaji

Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Mhandisi Rashid Kalimbaga kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa makalavati eneo la Manzase na uinuaji wa tuta ili kuondoa changamoto ya kujaa kwa maji katika eneo hilo hasa kipindi cha mvua.