WATUMISHI TANROADS ZINGATIENI SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO YA UTUMISHI WA UMMA KUEPUKA MIGOGORO
Dar es salaam
06/02/2026
Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, Februari 04, 2026, amefungua rasmi kliniki maalum ya masuala ya kiutumishi inayolenga kuongeza ufanisi na kupunguza migogoro inayokwamisha taasisi kufikia malengo yake.
Akizungumza katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam, Mhandisi Besta amesema kliniki hiyo imelenga kuwapa watumishi fursa ya kukutana na viongozi na wataalamu wa masuala ya utumishi ili kero zao zipatiwe majibu kwa wakati.
Aidha, amewahimiza watumishi kuzingatia maadili, sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kulinda taswira ya taasisi na kuepuka migogoro na migongano ya kimaslahi.
Naye Meneja Rasilimaliwatu wa TANROADS, Ndugu Pilika Kasanda, amesema kliniki hiyo itasaidia kujibu maswali ya kiutumishi na kuwataka watumishi kuwa huru kuwasilisha kero na maoni yao kwa lengo la kupata ufumbuzi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Makao Makuu, Mhandisi Donatus Dominick ameipongeza menejimenti kwa kutoa jukwaa la kusikiliza changamoto za watumishi, akisema hatua hiyo inapunguza manung’uniko kupitia majadiliano.
Kliniki hiyo ya siku mbili imewashirikisha zaidi ya watumishi na viongozi 200 wa TANROADS Makao Makuu na inatarajiwa kuendelea katika mikoa yote nchini, ambapo jumla ya watumishi 3,200 watanufaika