News

TANROADS YAWATAKIA HERI WATUMISHI WAO WAPYA

TANROADS YAWATAKIA HERI WATUMISHI WAO WAPYA

Dar es salaam.

19/01/2026

Wakala ya barabara (TANROADS) imehitimisha mafunzo yake rasmi  tarehe 17.1.2026 kwa watumishi wapya wa umma waliopata nafasi yakujiunga na TANROADS. Mafunzo hayo yaliyochukuwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 13.1.2026.

Akihitimisha mafunzo hayo Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mha. Ephatar Lucas Mlavi, ameleza kuwa watumishi hawa wapya ambao ni 136 watasaidia kuendesha kazi zetu kwa ufasaha kwani wengi ni vijana na wataweza kuitumikia serikali vizuri kupitia TANROADS.

Mha. Mlavi aliwapongeza watumishi hao wapya kwa kuweza kupata nafasi hizo, na kuwaambia kuwa haikuwa kitu chepesi kuweza kufika hapo walipo maana mliweza kupita katika mitihani ambayo imeendeshwa na Ofisi ya Raisi Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma.

“Ni imani yangu kwakweli mchuano haukuwa mdogo lakini mliweza kupambana na mwisho wa siku mkachaguliwa kujiunga na TANROADS niwape pongezi kwa hilo”. alisema Mha. Mlavi

Aliongeza kuwa wakala ya barabara (TANROADS) imekuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza maendeleo ya Taifa na ni miongoni mwa taasisi chache za serikali ambayo watumishi wake wanajituma na wana moyo wa kufanya kazi ili kuhakikisha wanaleta mchango katika taifa.

Aidha Mha. Mlavi alieleza kwamba anaamini kuwa watumishi hawa wapya watakuwa moja kati ya wafanyakazi ambao wataongeza nguvu katika sekta yao ili iweze kutimiza malengo kwa usahihi hasa ya ujenzi wa barabara zenye ubora unaotakiwia.

Hata hivyo Mha. Mlavi amewataka watumishi hao wapya kuyaishi na kuya zingatia yale yote waliyo fundishwa na kuelekezwa katika mafunzo hayo kwani ni vitu vya msingi na ndivyo ambavyo watatakiwa kwenda kuvifanya pindi watakapo kuwa makazini. Pia aliwataka kuwa makini sana wakati wanapotoa taarifa zinazo ihusu serikali.

“Mmeelekezwa umuhimu wa kulinda taarifa nyeti za serikali na kuepuka uvujishaji wa taarifa za serikali ambazo zinaweza zika athiri usalama wa nchi au maslai mapana ya umma, hili ni eneo muhimu sana hasa katika nyakati hizi za utandawazi ambapo taarifa inaweza ikatumiwa vibaya mara nyingine”. alisema Bw. Mlavi

Aidha Mha. Mlavi alibainisha kuwa wamewaajili watumishi wengi kwa lengo la kwenda kuongeza nguvu kazi katika sekta au vituo vya mizani vya upimaji wa magari, na kupitia mafunzo haya mmepata fursa yakufahamu kanuni na sheria za uwendeshaji wa vituo hivyo.

Aliongeza nakusema kuwa barabara nimoja kati ya miliki yenye thamani ambayo serikali inamiliki, hivyo mizani imewekwa kwaajili ya kuhakikisha barabara inalindwa na kutumika kwa matumizi yasiyoweza kuiharibu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Elirehema Obed Saiteru, alisema anawakaribisha sana, na kuwahasa wasiwe na haraka na kuwa na maisha mazuri bali wawe wavumilivu na kuzingatia yale ambayo wamefundishwa. 

Naye Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka TANROADS Bi. Fatima Kasimu Matimba alisema haikuwa rahisi kuwapata watumishi hawa kwani walikuwa wengi lakini kupitia Sekretarieti ya Ajira imefanya kazi yake na kuweza kutupatia watumishi hawa.