News

TANROADS YASHIRIKI UZINDUZI WA BARABARA YA KIZIMKAZI ZANZIBAR KM 6.72 

TANROADS YASHIRIKI UZINDUZI WA BARABARA YA KIZIMKAZI ZANZIBAR KM 6.72 Zanzibar, 11 Januari, 2026 Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) hivi karibuni wameshiriki kikamilifu uzinduzi wa barabara za Kizimkazi zenye urefu wa Km. 6.72 zilizopo Mkoa wa Kusini Unguja. Sherehe hizo za ufunguzi wa barabara hiyo imefunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma, aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Suleiman Masoud Makame na kwa upande wa TANROADS zimeudhuriwa na watumishi saba walioongozw ana Meneja wa Mazingira na Jamii, Bi. Zafarani Madayi kwa niaba ya Mtendaji Mkuu Mhandisi Mohamed Besta. Barabara hizo zimejengwa kwa kiwango cha lami kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS), ambapo Mhe. Hamza amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imejidhatiti kujenga barabara za lami Mjini na vijijini ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta maendeleo. Mhe. Hamza amesema ujenzi wa miundombinu unaofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatekeleza malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo katika sherehe za mwaka huu zilizofanyika tarehe 12 Januari, 2026  ikiwa ni miaka 62 kaulimbiu yake ni “Amani na Umoja ndio Msingi wa Maendeleo Yetu”, ambapo pia amewataka wananchi na madereva hususan waendasha bodaboda kuzitunza na kuzitumia kwa uangalifu ili kuepusha ajali na zidumu kwa muda mrefu. “Jeshi la Polisi lichukue hatua za kisheria ikiwemo faini kwa madereva wanaopakia nondo na kuziburura njiani jambo ambalo linaharibu barabara zinazoendelea kujengwa na zilizokamilika kujengwa,” amesema Mhe. Hamza.