News

WAZIRI MKUU AIAGIZA WIZARA YA UJENZI KUHARAKISHA USANIFU BARABARA MKOANI MBEYA

WAZIRI MKUU AIAGIZA WIZARA YA UJENZI KUHARAKISHA USANIFU BARABARA MKOANI MBEYA

Mbeya, 18 Desemba, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha usanifu wa barabara ya Kiwira - Isangati na Kimo - Kafwafwa KM 22 unakamilika ifikapo mwezi April mwakani.

Amesema hayo alipokagua miundombinu mkoani Mbeya na kusisitiza ujenzi wa barabara hiyo uanze mara moja baada ya usanifu kukamilika.

"Hakikisheni mnawasimamia vizuri wakandarasi na kufanya tathmini ili kazi inayofanywa iendane na thamani ya fedha", amesema Dkt. Mwigulu.

 Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Wizara imejipanga vizuri kuhakikisha usanifu wa barabara mkoani Mbeya unakamilika kwa wakati.