News

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA LINDI.

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MADARAJA LINDI.

l Asisitiza Rais Dkt. Samia amedhamiria kushughulika na changamoto za watanzania

Lindi, 19 Desemba, 2025

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa madaraja na ukarabati wa barabara kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaambia wakazi wa Somanga mkoani Lindi kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi ya kimkakati ili kushughulika kwa vitendo na umasikini wa Watanzania

Aidha, Dkt. Mwigulu ameipongeza Wizara ya Ujenzi, Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakandarasi wote waliotelekeleza ujenzi wa madaraja hayo pamoja na Jeshi la Polisi kwa kuratibu na kusimamia ulinzi na usalama wa wananchi wakati wa adha ya uharibu ya miundombinu hiyo kipindi cha mvua za El- Nino na Kimbunga Hidaya.

Dkt. Mwigulu ameridhishwa na hatua za maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa madaraja ya dharura (CERC) Mkoani Lindi ambapo utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 90 na kuhakikishiwa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kuwa sasa wananchi watapita juu ya madaraja katika misimu ya mvua zijazo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema ukamilishaji wa daraja la Somanga Mtama (M60) utaenda sambamba na uwekaji wa taa za barabarani ili kuendelea kurahisisha shughuli za kibiashara kufanyila nyakati zote.