News

UJENZI WA BARABARA YA LAMI RUANDA–IDIWILI (KM 20) WAENDELEA, TAA ZA BARABARANI NA AJIRA ZA WANANCHI KIPAUMBELE 

UJENZI WA BARABARA YA LAMI RUANDA–IDIWILI (KM 20) WAENDELEA, TAA ZA BARABARANI NA AJIRA ZA WANANCHI KIPAUMBELE 

Songwe, 14 Desemba, 2025

Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kipande cha Ruanda hadi Idiwili chenye urefu wa kilometa 20 unaendelea tangu kuanza kwake mwezi Agosti mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya mradi huo, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amesema Rais Samia ameridhia ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa barabara zote zinazojengwa kwa sasa lazima zikamilike kwa viwango vya juu, ikiwemo uwekaji wa taa za barabarani.

Amesema uwekaji wa taa hizo utaimarisha usalama na kuwawezesha wananchi wa Iyula na vijiji jirani kufanya shughuli za biashara mchana na usiku. 

Mhe. Ulega amesema ameridhishwa na kasi na ubora wa kazi inayoendelea hadi sasa, huku akiwataka wakandarasi wanawake wanaotekeleza mradi huo kushiriki kikamilifu katika kusimamia na kuhakikisha barabara inakamilika kwa wakati ili iwe chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo na Taifa kwa ujumla.

Amepongeza pia hatua ya wakandarasi hao kutoa ajira kwa vijana wa maeneo husika, akisisitiza kuwa vijana wote wanaofanya kazi wapewe vyeti vya kuthibitisha ushiriki na uzoefu wao mara baada ya kukamilisha kazi, ili viwasaidie kupata fursa nyingine za ajira katika miradi ijayo. 

Waziri Ulega amebainisha kuwa, Serikali itaendelea kusimamia mradi huo kwa karibu kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), akiwataka Mameneja wa mikoa ya Songwe na Mbeya kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa ufanisi na bila kasoro, huku Serikali ikihakikisha fedha za ujenzi zinapatikana kwa wakati.

 Kwa upande wake, aliyekuwa Meneja TANROADS Mkoa wa Songwe ambaye sasa amehamishiwa katika Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujenga barabara ya lami kutoka Ruanda hadi Ituba yenye jumla ya kilometa 79 ambapo ameeleza kuwa sehemu ya kwanza ya mradi huo yenye urefu wa kilometa 20 ndiyo inayoendelea kujengwa kwa sasa.

Mhandisi Bishanga amesema ujenzi wa kipande hicho unatekelezwa na wakandarasi wanawake kutoka maeneo mbalimbali, ambapo kila mkandarasi amepangiwa kujenga kilometa tano tano.

Ameongeza kuwa mradi ulikabidhiwa rasmi kwa wakandarasi Agosti 12, 2025, na kuishukuru Serikali kwa kuwawezesha wakandarasi wanawake pamoja na kulipa fedha kwa wakati, hali inayochochea maendeleo mazuri ya kazi. 

Naye Rais wa Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania (TWCA) Mhandisi Judith Odunga, amesema hadi kufikia sasa mradi umefanikiwa kutoa ajira 240, zikiwemo ajira 36 kwa wanawake na 204 kwa wanaume.

 Ameeleza kuwa idadi ya ajira itaendelea kuongezeka kadri ujenzi unavyoendelea, huku wafanyakazi wote wakiwa ni Watanzania, wengi wao wakitoka maeneo ya Iyula hadi Ileje.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Ruanda–IdiwiIi unatarajiwa kuimarisha usafiri, kukuza biashara, kuongeza usalama na kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe n