News

KATIBU MKUU UJENZI ASISITIZA MSALATO AIRPORT KUKAMILIKA KWA WAKATI

KATIBU MKUU UJENZI ASISITIZA MSALATO AIRPORT KUKAMILIKA KWA WAKATI

Dodoma, 02 Desemba, 2025

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour amekagua utekelezaji wa mradi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma, na kusisitiza mradi huo ukamilike kwa wakati.

 Aidha, ameelekeza kwa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) pamoja na Mhandisi Mshauri kuhakikisha kuwa wanamsimamia Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group Company Ltd ( BCEG) katika ujenzi wa sehemu ya pili inayohusisha jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na majengo mengine kuongeza kasi ya utekelezaji ili majengo hayo yakamilike kama ilivyopangwa kwenye mkataba.

Mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato unatazamiwa kufungua fursa za kiuchumi na kijamii na hivyo kuleta maendeleo jijini Dodoma na Taifa kwa ujumla pindi utakapokamilika.