News

MHE. ULEGA NA MHANDISI KASEKENYA WAAPA RASMI KUWA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA UJENZI

MHE. ULEGA NA MHANDISI KASEKENYA WAAPA RASMI KUWA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA UJENZI

Dodoma, Novemba 18, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha rasmi Mhe. Abdallah Ulega na Mhandisi Geofrey Kasekenya kuendelea na wadhifa wao wa Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.

Mhe. Ulega, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, amerudishwa kwenye nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa mafanikio katika Baraza la Mawaziri lililopita.

Pia Mhandisi Kasekenya amerejea kwenye nafasi ya Unaibu Kuendelea kwao kuaminiwa na kupewa dhamana hii kunadhihirisha umuhimu wa kuimarisha mwendelezo wa utekelezaji wa sera, mipango na mikakati ya Serikali katika sekta ya ujenzi.

Ni hatua inayoonyesha dhamira ya Serikali ya kuweka wasimamizi makini, wabobezi na mwenye uzoefu kama Mhe. Ulega na Mha. Kasekenya ili kuhakikisha usimamizi madhubuti wa miradi ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege, sambamba na kuhakikisha matokeo ya maendeleo yanafikiwa kwa wakati, kwa viwango vinavyokusudiwa na kuwafikia wananchi moja kwa moja.