News

MAAFISA MAWASILIANO WANOLEWA KUHUSU MATUMIZI YA AKILI UNDE (AI) KWENYE MIFUMO YA KIDIJITI KATIKA MAWASILIANO YA SERIKALI.

MAAFISA MAWASILIANO WANOLEWA KUHUSU MATUMIZI YA AKILI UNDE (AI) KWENYE MIFUMO YA KIDIJITI KATIKA MAWASILIANO YA SERIKALI.

 Arusha, 11 November,2025

Chama cha Maafisa Mawasiliano ya Serikali kimeandaa mafunzo kwa wanachama wake kuhusu matumizi ya akili unde (Artificial Intelligence) kwenye mawasiliano kidijitali katika utekelezaji wa kazi za habari na mawasiliano ya Serikali.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mwenyekiti wa TAGCO, Katibu Mwenezi Msaidizi wa Chama hicho Bw. Kassim Nyaki ameeleza kuwa uendeshaji wa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa chama hicho kuwezesha wanachama wake kupata mbinu za kisasa katika utekelezaji wa majukumu ya kuisemea Serikali na kuwasiliana na Umma kupitia huduma mbalimbali na miradi ya Miundomnibu inayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya manufaa kwa Wananchi.

“Mafunzo haya yanajikita katika matumizi ya akili Unde hususan mawasiliano ya kimkakati katika mifumo ya kidijitali, kuandaa mawasiliano na uhusiano kwa umma kimkakati, namna ya kutumia akili unde kama nyenzo ya kukabiliana na mitazamo mbalimbali katika jamii na kuisaidia jamii kupata habari sahihi, za uhakika kwa muda ili kuepukana na habari zenye kupotosha” alisisitiza Nyaki

Moja ya mshiriki wa Mafunzo hayo Bi. Jamillah Mbarouk, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Taasisi ya Elimu Tanzania  ameeleza kuwa kutumia “Articifial Intelligence” inawasaidia maafisa Mawasiliano wa Serikali kuchambua  ni maudhui gani ya kufikishia Umma kwa wakati na kuweza kudadavua mbinu sahihi na salama za kufikisha taarifa kwa wananchi ambapo ametumia fursa hiyo, kushukuru uongozi wa TAGCO kwa kuandaa mafunzo hayo ili kuwaongezea ufanisi na tija katika kuboresha kazi za kihabari kwenye taasisi za Serikali kwa maslahi ya watanzania kwa Ujumla.