TECU YAKAGUA MIRADI YA CERC MANYARA
Manyara, 12/10/2025
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Miradi (TECU), Mhandisi Lutengano Mwandambo, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (CERC) katika Mkoa wa Manyara.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Mwandambo alikagua mradi wa ujenzi wa daraja katika eneo la Minjingu, ambapo alimpongeza mkandarasi Roctronic kwa kutekeleza kazi kwa kuzingatia ubora na muda uliopangwa.Katika ukaguzi huo, Mhandisi Mwandambo aliambatana na timu ya wahandisi kutoka Ofisi ya Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Manyara, wakiongozwa na Mhandisi mkazi wa miradi hiyo, Charles Lyamuya.
Mbali na mradi wa Minjingu, Mhandisi Mwandambo alitembelea pia mradi wa ujenzi wa daraja eneo la Kateshi, ambako alionesha kuridhishwa na hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
Aidha, aliwapongeza wahandisi kutoka Ofisi ya Meneja wa TANROADS na timu ya TECU kwa usimamizi mzuri na ufuatiliaji makini unaochangia miradi hiyo kufikia viwango vya kuridhisha vya utekelezaji.