News

UJENZI WA BARABARA YA KAHAMA-KAKOLA WAFIKIA ASILIMIA 45.16

UJENZI WA BARABARA YA KAHAMA-KAKOLA WAFIKIA ASILIMIA 45.16

Kahama

02 Oktoba, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Mboni Mhita amefanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Kakola (Km 73) kwa kiwango cha lami na kupongeza hatua za utekelezaji wa mradi huo.

Akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joel Mwambungu, amesema ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 45.16, ambazo ni mbele ya mpango kazi wa asilimia 43.74, hivyo kupelekea uwezekano wa kukamilisha mradi kabla ya kipindi cha mkataba kukamilika.