News

TANROADS YAENDELEA KUTATUA KERO YA MUDA MREFU YAJENGA DARAJA ENEO LA SITALIKE

TANROADS YAENDELEA KUTATUA KERO YA MUDA MREFU YAJENGA DARAJA ENEO LA SITALIKE

Katavi

12 Sept, 2025

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wameeleza furaha na shukrani zao kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutatua kero ya muda mrefu kwa kujenga daraja kubwa katika eneo la Sitalike.

Kwa miaka mingi, eneo hilo limekuwa likikumbwa na mafuriko hasa nyakati za masika, hali iliyosababisha usafiri kusimama mara kwa mara. Mwaka uliopita, mvua kubwa za El Niño zilisababisha daraja la awali kubomoka kabisa na kusitisha safari kati ya Katavi na Rukwa.

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imejibu changamoto hiyo kwa kujenga daraja jipya na la kudumu, litakalowawezesha wananchi kusafiri bila usumbufu na kufanikisha shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa uhakika zaidi.

Wananchi wa Sitalike wamesema ujenzi huu ni suluhisho muhimu kwa maisha yao ya kila siku na ushahidi wa jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya barabara nchini