News

UJENZI WA KAHAMA-KAKOLA KUTEKELEZWA MCHANA NA USIKU

UJENZI WA KAHAMA-KAKOLA KUTEKELEZWA MCHANA NA USIKU 

Kahama

08/09/2025

Kazi za ujenzi wa barabara ya Kahama–Kakola zenye urefu wa kilomita 73 zinaendelea kwa kasi usiku na mchana chini ya usimamizi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).Mradi huu wa kimkakati unalenga kuondoa changamoto ya muda mrefu ya usafiri katika eneo hilo, sambamba na kufungua fursa mpya za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa mikoa ya Shinyanga na Geita.

Kupitia barabara hii, shughuli za biashara, usafirishaji wa bidhaa, na huduma za kijamii zinatarajiwa kuimarika kwa kiwango kikubwa, na hivyo kuongeza mchango wa sekta ya miundombinu katika maendeleo ya taifa.