WAKANDARASI NA WAHANDISI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAZINGIRA MANYARA
Manyara
19 Agosti, 2025
Wakandarasi na Wahandisi wa ujenzi mkoani Manyara wamepatiwa mafunzo ya siku tatu kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya mazingira na kijamii katika utekelezaji wa miradi ya barabara.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Manyara, na yamehusisha wahandisi wa TANROADS na wale kutoka kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi mingi ya ujenzi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Meneja Msaidizi wa TANROADS Mkoa wa Manyara, Mhandisi Greyson Ndyamukama, amesema elimu hiyo imetoa mwanga kwa washiriki kuona namna mazingira na masuala ya kijamii yanavyotakiwa kupewa kipaumbele katika miradi ya ujenzi wa miundombinu za barabara na madaraja.
“Semina hii imetupa mwanga wa kuona umuhimu wa mazingira katika utekelezaji wa miradi yetu pamoja na masuala ya kijamii,” alisema Mha. Ndyamukama.
Mafunzo hayo ambayo pia yamefundishwa pia kwa vitendo kwa washirik.i kutembelea baadhi ya miradi, yameongozwa na mtaalamu wa mazingira na masuala ya kijamii kutoka Benki Kuu ya Dunia, Bw. Gasper Mashingira