News

RC MANYARA AKAGUA UJENZI WA KALVATI ENEO LA MSASANI BABATI

RC MANYARA AKAGUA UJENZI WA KALVATI ENEO LA MSASANI BABATI

Manyara

03 Julai, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Box Culvert (daraja dogo) unaoendelea katika Barabara Kuu ya Babati–Arusha, eneo la Msasani, Wilaya ya Babati.Katika ziara hiyo, aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati.

Amesema ameamua kufanya ukaguzi huo kwa kuwa mradi huo uko kwenye barabara kuu inayounganisha mikoa ya Dodoma, Singida na Arusha, na hivyo ni muhimu kwa uchumi na usafirishaji wa watu na bidhaa.

Mheshimiwa Sendiga ameipongeza Ofisi ya Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Manyara kwa kusimamia vizuri mradi huo na kuhakikisha unatekelezwa kwa wakati.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufuatilia miradi yote ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.