News

RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI DARAJA LA J.P MAGUFULI

RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI DARAJA LA J.P MAGUFULI

 Mwanza

19 Juni, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 19, 2025, ameongoza hafla ya uzinduzi rasmi wa daraja la J.P. Magufuli lililopo mkoani Mwanza, mradi mkubwa wa miundombinu lenye urefu wa kilomita 3 pamoja na barabara unganishi yenye kilometa 1.6.

Daraja hili la kihistoria limejengwa kwa lengo la kuimarisha mtandao wa barabara kati ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na Shinyanga na pia kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Hii ni hatua kubwa kuelekea kukuza biashara za kikanda, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi kwa ujumla.