News

SERIKALI INAFANYA USANIFU WA KINA BARABARA YA CHALINZE-SEGERA

SERIKALI INAFANYA USANIFU WA KINA BARABARA YA CHALINZE-SEGERA

 

Dodoma

06 Mei, 2025

Serikali ya Awamu ya sita kupitia kwa Wizara ya Ujenzi imeliambia Bunge la Tanzania tarehe 06 Mei, 2025 kuwa kwasasa unafanyika usanifu wa kina kwenye Barabara ya Chalinze- Segera Mkoani Tanga, ili kuanza upanuzi wa barabara hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanga na mikoa ya Kaskazini mwa nchi.Waziri Abdallah Ulega anayesimamia Wizara ya Ujenzi amebainisha hayo wakati akiihitimisha mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya wizara yake kwa Mwaka wa fedha 2025/26, akieleza kuwa serikali inatambua kuwa barabara hiyo imekuwa finyu kwasasa kutokana na wingi wa matumizi yake kwa kuwa ilijengwa miaka mingi iliyopita, hivyo kushindwa kukidhi haja na mahitaji ya sasa.Waziri Ulega ameeleza hayo kufuatia hoja na ushauri kadhaa uliotolewa na Wabunge akiwemo Mhe. Ummy Mwalimu (Mbunge wa Tanga Mjini) na Mhe. Rashid Abdallah Shangazi (Mbunge Jimbo la Mlalo) walioomba barabara hiyo kutazamwa kwa kina na Wizara ambapo Mhe. Ulega ameahidi kuwa mara baada ya usanifu, mchakato utakaofuata ni kutafuta fedha kwaaajili ya Ujenzi wa barabara hiyo.