News

TANROADS YASAINI MIKATABA NA WASHAURI ELEKEZI WA MIRADI YA TanTip

TANROADS YASAINI MIKATABA NA WASHAURI ELEKEZI WA MIRADI YA TanTip

 

Dar es Salaam

13 Septemba, 2024

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Septemba 13, 2024 imetiliana saini mikataba miwili na Mshauri Elekezi, kampuni ya Dar Al-Handasah Consultant kwa ajili ya kazi ya kusimamia miradi miwili, ambayo iko chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) yenye miradi saba (7) nchini ya TanTip hapa nchini inatekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta akiongea katika hafla hiyo ambapo ameagiza kuwa ndani ya mwezi Septemba na Oktoba, mwaka 2024 miradi ya TanTip iwe imekamilika kusainiwa.

Mhandisi Besta amesema kuwa, tarehe 21 Septemba, 2024 kutakuwa na hafla ya zoezi la kutiliana saini na mkandarasi kwa ajili ya kazi za ujenzi wa barabara ya Iringa hadi Msembe yenye urefu wa Kilometa 104 kwa kiwango cha lami.

Mbali na miradi hiyo, TANROADS pia imesaini vipande viwili vya mradi wa ujenzi wa daraja barabara ya Mtwara - Mingoyo - Masasi yenye urefu wa
Kilometa 200 ambayo inasimamiwa na Mshauri Elekezi kampuni ya Dar Al-Handasah Consultant, ambapo Mshauri Elekezi huyu anatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi kwenye wizara nyingine hapa nchini na pia Zanzibar