News

Waziri Mhe. Bashungwa aelekeza TANROADS kukutana na Mameneja wa madini mikoani

Njombe,

25 Januari, 2024

 

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ametoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta kupitia kwa Mameneja wa TANROADS wa Mikoa yote Nchini; kukaa na Meneja wa Wizara ya Madini wa Mikoa husika kuangalia namna nzuri ya kuwezesha upatikanaji wa Milima ya kupata nyenzo za kujenga miradi ya barabara ikiwemo Mawe na Kokoto.

 

Amesema kwa sasa Milima yote yenye mawe ya kukata kokoto kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ya barabara ipo mifukoni mwa watu ni kama Vishoka wanapata lesini alafu wanazikalia, TANROADS ikipata Mkandarasi inatafuta eneo la kukata mawe ili ikatengeneze barabara wahusika wanataja fedha ambazo ukizilipa zinaongeza gharama za mradi jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa Nchi nzima.

 

Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo tarehe 24 Januari 2024 wakati akitoa taarifa ya majumuisho ya ziara yake Mkoani Njombe mbele ya Uongozi wa Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Njombe muda mfupi kabla ya kuelekea Mkoani Ruvuma ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TANROADS kuanzia kesho tarehe 25 Januari 2025.

 

Amewataka Meneja hao kukaa pamoja kuangalia namna ambavyo TANROADS inaweza kuomba leseni kupata Milima hiyo katika maeneo ambayo kuna miradi ya kimkakati ili inapopata Mkandarasi isipate shida ya kwenda kutafuta watu ambao ni Vishoka wanaouza Milima hiyo kwa fedha nyingi na hivyo kuongeza gharama za Ujenzi wa miradi na kusababisha ucheleweshwaji wa kukamilika kwa miradi.

 

"Taarifa hiyo ikishakamilika Mkaleta kwangu ninaweza kwenda kwa bosi wangu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko nikamwambia ona hali ilivyo vishoka wamezidi Mikoa yote wameshikilia milima tunashindwa kujenga barabara kwa sababu tunakosa sehemu za kupata kokoto na nyenzo za ujenzi wao ni Vishoka ambao wanasubiri kuna mradi flani wanakimbilia kushika milima ukimuliza hizo kokoto tunazinunua kwa bei gani wanakutajia mabilioni ya fedha.