News

WALIOPISHA UJENZI WA BARABARA YA MTWARA-MINGOYO-MASASI KULIPWA FIDIA

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe. Deogratius Ndejembi kuwa wananchi wote wanaodai fidia kupisha ujenzi wa Barabara ya Mtwara- Mingoyo- Masasi km 200 watalipwa stahiki zao mwezi Desemba mwaka huu.

Amesema hayo jimboni Mtama alipokuwa akijibu ombi la Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye aliyetaka kujua fidia hizo zitalipwa lini.

" Mhe Makamu wa Rais kiasi cha shilingi milioni 819 zitalipwa Desemba 5, mwaka huu kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara hii", amesisitiza Eng. Kasekenya.

Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara za kisasa katika mikoa ya kusini (Ruvuma, Mtwara na Lindi), na kusisitiza zitachochea ukuaji wa kilimo na biashara na kuongeza mapato kwa wananchi.

Makamu wa Rais Mhe. Ndejembi ambaye anaendelea na ziara katika mikoa ya kusini, ameanza ziara katika mkoa wa Lindi baada ya kumaliza mkoani Mtwara.