News

TANROADS YAADHIMISHA SIKU YA WAHANDISI, YATOA WITO WA UBUNIFU KATIKA MIUNDOMBINU

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka Wahandisi nchini kuendana na teknolojia ya akili unde ili kukuza ubunifu, ujuzi na kufanikisha Dira ya Tanzania ya 2050.Huku akiwataka  wahandisi nchini kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao.

Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wahandisi, ambapo amewasihi kupiga vita uzemba na rushwa huku wakisimamia viwango vya juu vya kulinda taaluma yao.

Katika kuadhimisha Siku ya Wahandisi Duniani nchini Tanzania – Engineers’ Day 2026, Tanzania National Roads Agency (TANROADS) inaungana na wahandisi na wadau wa sekta ya uhandisi kutambua mchango muhimu wa taaluma hiyo katika maendeleo ya taifa, hususan katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara.

Maadhimisho ya 23rd Annual Engineers’ Day 2026, yanayofanyika jijini Dar es Salaam, yamebeba kaulimbiu “Leveraging Engineering Innovation and Digital Transformation for Sustainable Development”, inayosisitiza matumizi ya ubunifu wa kihandisi na mabadiliko ya kidijitali katika kuleta maendeleo endelevu.

Kwa upande wa TANROADS, wahandisi wameendelea kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya barabara na madaraja, usimamizi wa matengenezo, matumizi ya teknolojia katika ujenzi na usimamizi wa miundombinu, pamoja na kuhakikisha ubora, usalama na uimara wa miundombinu ya barabara nchini.

TANROADS inaendelea kuhimiza matumizi ya teknolojia, ubunifu na utaalamu wa kihandisi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za miundombinu na kujenga mtandao wa barabara unaokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.

TANROADS inawatakia wahandisi wote nchini Tanzania maadhimisho mema ya Engineers’ Day 2026.