News

TANROADS YAWEK A MIKAKATI KUDHIBITI MAFURIKO JANGWANI DAR ES SALAAM.

 Septemba 2026.

 Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imechukua hatua za kimkakati katika eneo la Jangwani, Dar es Salaam, kuongeza uwezo wa maji kupita kwa haraka na kupunguza athari za mafuriko wakati wa mvua kubwa.

Mhandisi wa Kitengo cha Usalama Jangwani, Samueli Nyari, amesema hatua hizo ni pamoia na ujenzi wa diversion road ilivyoinuliwa hadi takribani mita saba kutoka usawa wa bahari na daraja jipya enye kiwango cha takribani mita 8.4, ikilinganishwa na mita sita za daraja la awali.

Amesema daraja jipya limejengwa kwa nafasi na kiwango kinachowezesha maji kupita kwa wingi na kwa haraka.

 TANROADS pia inaendelea kusafisha Mto Jangwani upande wa juu na chini wa daraja na kubomoa daraja la zamani ili kuondoa vizuizi cha mtiririko wa maji Aidha, imejenga makalavati yenye midomo sita katika maeneo mawili, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa kupitisha maji na kupunguza maji kutuama katika maeneo ya barabara.,

Mkaguzi wa Kazi katika Mradi wa Daraja la Jangwani, Mhandisi Kelvin Mwabulanga, amesema maeneo muhimu ya mradi, ikiwemo ofisi na Batch Plant, zimejengwa kwenye mwinuko salama, huku tuta la barabara likiinuliwa zaidi kulinda watu na vifaa endapo kiwango cha maji kitaongezeka.

"Kwa sasa tunaendelea na kazi va kubomoa daraja la zamani ili kuongeza nafasi ya maji kupita kwa wingi na kwa haraka katika Mto Jangwani," amesema Mhandisi Mwabulanga.

TANROADS imewataka wananchi kutotupa taka kwenye mito, mifereii, makalavati na maeneo ya kupitisha maji, kwani zinaweza kuziba njia za maji na kuongeza hatari za mafuriko. Madereva na watumiaji wa barabara pia wametakiwa kufuata maelekezo ya mamlaka husika na kutumia njia mbadala wakati wa mvua kubwa.