Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Meneja wake, Mha. Elsony Mweladzi, umekutana na Wakandarasi zaidi ya 16 wanaotekeleza miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo, kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa kazi, kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, pamoja na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.
Katika kikao hicho, TANROADS Mkoa wa Kigoma imewapatia Wakandarasi hao mwongozo kuhusu namna bora ya kutekeleza miradi waliyopewa, huku ikisisitiza umuhimu wa kuzingatia masharti ya mikataba, kanuni, taratibu na sheria zinazohusiana na utekelezaji wa miradi ya barabara.
Aidha, kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa pamoja kati ya TANROADS na Wakandarasi, kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi na kuweka mikakati ya kuhakikisha kazi zinakamilika kwa wakati, kwa ubora unaohitajika na kwa kuzingatia thamani ya fedha za Serikali.
Kwa upande wao, Wakandarasi hao wameishukuru TANROADS Mkoa wa Kigoma kwa kuwaalika na kuwapatia mwongozo wa kina kuhusu namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Wamesema maelekezo hayo yatawasaidia kuongeza ufanisi na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa weledi, ubora na kwa kuzingatia sheria pamoja na masharti ya mikataba.
Wakandarasi hao pia wameahidi kushirikiana kwa karibu na TANROADS katika kuhakikisha miradi waliyopewa inatekelezwa kwa weledi na uwajibikaji, huku wakizingatia viwango na taratibu zote zilizowekwa.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za TANROADS Mkoa wa Kigoma katika kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya barabara, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata miundombinu bora na salama, na kwamba miradi ya Serikali inatekelezwa kwa ufanisi, kwa kuzingatia thamani ya fedha