News

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AIPONGEZA TANROADS KWA UJENZI WA BARABARA BORA

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AIPONGEZA TANROADS KWA UJENZI WA BARABARA BORA

Dodoma

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, ameipongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kazi kubwa ya kujenga na kusimamia mtandao wa barabara unaohudumia Tanzania na nchi jirani katika usafirishaji wa abiria na mizigo.

Dkt. Msonde alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la TANROADS katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma.

Amesema barabara kama TANZAM zina mchango mkubwa katika kukuza biashara na uchumi wa Tanzania na ukanda wa Afrika Kusini na Mashariki.

Pia amepongeza TANROADS kwa kuhakikisha ubora wa barabara kupitia ukaguzi wa kitaalamu na kuwataka kuendelea kuimarisha usimamizi wa miradi ili kuhakikisha kazi zinakidhi viwango.Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufanya matengenezo ya barabara kwa wakati ili kulinda uwekezaji wa Serikali na kuongeza maisha ya miundombinu hiyo.

Dkt. Msonde pia amekipongeza Kitengo cha Utafiti na Maendeleo cha TANROADS kwa huduma za upimaji wa malighafi za ujenzi na kuwahimiza wananchi kutumia maabara za TANROADS kupima mchanga, kokoto, nondo, udongo na vifaa vingine kabla ya kuanza ujenzi.

Amesema hatua hiyo itasaidia kujenga majengo salama na yenye ubora, huku akihimiza ushirikiano kati ya TANROADS na taasisi nyingine za sekta ya ujenzi ili kuongeza ubora wa miundombinu nchini