News

BARABARA YA MCHEPUO YA UYOLE KUPUNGUZA FOLENI MBEYA

BARABARA YA MCHEPUO YA UYOLE KUPUNGUZA FOLENI MBEYA

Dodoma, 21 Mei, 2026

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida Patali ameipongeza serikali kupitia Wakala ya Barabara ya Tanzania (TANROADS), kwa kujenga miundombinu bora ya barabara.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi katika Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea jijini Dodoma leo tarehe 21 Mei, 2026, Patali amesema jiji la Mbeya lina barabara kubwa moja ya TANZAM.

“Nampongeza Meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya Mhandisi Bishanga kwa usimamizi wake makini,” amesema Patali

Hatahivyo, ametoa ushauri kuwa barabara ya mchepuko ya kutoka Uyole kupitia kata ya Swae kwenda hadi Songwe ianze kujengwa sasa ili kupunguza msongamano katikati ya jiji la Mbeya.

Pia amesema mchepuko huo utasaidia kuharakisha ujenzi wa barabara kutokana na kuwa magari machache kupita kwenye njia kuu, na pia itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara kwa kuwa magari makubwa ya mizigo yatapita kwenye mchepuko huo.