News

UJENZI WA BARABARA YA RWAMISHENYE-BUKOBA PORT (Km5.1) KWA NJIA NNE WASHIKA KASI

UJENZI WA BARABARA YA RWAMISHENYE-BUKOBA PORT (Km5.1) KWA NJIA NNE WASHIKA KASI

Kagera, 14 Mei,2026

Ujenzi wa Barabara ya Rwamishenye- Bukoba Port (Km 5.1), Kipande cha Nyagowe hadi Bukoba Mjini (km 1.6) kwa Njia Nne upo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake. Haya yamesemwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Mha SAMWEL Joel MWAMBUNGU alipokuwa akitoa Taarifa kwa wandishi wa Habari na kushuhudiwa uwekaji waTabaka la Lami ukiendelea na hatua za ujenzi zikiwa takribani asilimia 90

Ujenzi wa Barabara hii umezingatia viwango vya kimataifa na matumizi ya Teknolojia ya Kisasa “Superpave” katika Ujenzi wa Tabaka la Lami hivyo kufanya Barabara hii kuwa ya viwango vya kimataifa, amesema Mha Mwambungu.

Mbali na Ujenzi wa Km 1.6 kwa njia Nne kwa kiwango cha Lami, pia kuna Ujenzi wa Daraja la mto Kanoni ambalo limekalilika na uwakaji wa Jumla ya Taa 58 za kuleta mwanga wakati wa usiku.

Aidha, Mhandisi MWAMBUNGU amefafanunua kuwa, faida kuu za Mradi kuu ni pamoja na kufungua Lango la kiuchumi kwa Manispaa ya Kagera, lakini pia Ujenzi wa Barabara hii unatekelezwa na Mkandarasi  mzawa (Abemulo Contractors Ltd) hivyo kujenga uwezo na kutengeneza Ajira wa watanzania. Pia kabla ya Ujenzi  wa Barabara hii, kulikuwa na Ajali Nyingi sana kwenye Mlima Nyagowe na kupoteza maisha ya watanzania wengi sana, lakini kwa sasa Mlima umepunguzwa na kuondoa kabisa tatizo la Ajali zilizokuwa zinajitokeza.

Mhandisi MWAMBUNGU amewaasa Vijana wa Kagera kuchangamkia Fursa zitokanazo na uwezo wa Barabara ya njia Nne, kufanya biashara usiku na mchana, Kwani Mkoa wa Kagera ni kiungo muhimu cha Nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.