News

WAZIRI ISACK KAMWELWE AWASILI OFISINI JIJINI DODOMA LEO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amewasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara yake mjini Dodoma leo na kulakiwa na watumishi wa Sekta hizo.

Waziri Mhandisi Isack Kamwelwe, aliapishwa tarehe 02/07/2018 Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri tarehe 01/07/2018 ambapo aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alihamishiwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Waziri Mhandisi Kamwelwe, kabla ya kuwasili ofisini kwake alianza ziara ya kikazi katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Geita na Kigoma ambapo alitembelea na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na sekta hizo tatu hasa miundombinu ya barabara, bandari, vivuko, meli na reli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano