News

SAMIA: MADEREVA WA BODABODA ACHENI HARAKA.

Madereva wa Pikipiki (bodaboda) nchini wametakiwa kutii sheria za Usalama Barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi zinazotokea barabarani zimekuwa zikisababishwa na uzembe unaofanywa na madereva hao.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya wiki yanenda kwa usalama kitaifa mkoani Kilimanjaro Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa chanzo kikuu cha ajali hizo ni uharaka walionao madereva hao na ukosefu wa mafunzo ya usalama barabarani kwa baadhi ya madereva.

“Madereva wa bodaboda naomba mbadilike, muwe na tabia ya kutii sharia za usalama barabarani bila shuruti kwani ajali nyingi nchini zimekuwa zikisababishwa na nyinyi kutokana na harakaharaka zenu”, amesema MakamuRais.

Aidha, amefafanua kuwaTathmini iliyofanywa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu katika mkoa wa Kilimanjaro imebaini kuwa kuna ajali za Pikipiki 84 zilizojitokeza ambazo kati ya hizo, 61 zimesababisha vifo na zilizobaki majeruhi.

Kuhusu ajali za mabasi ya abiria Mheshimiwa Makamu wa Rais amesema kuwa zimepungua kutokana na uwepo wa mbinu za udhibiti wa mabasi hayo kama vile upigaji picha kwa magari yanayozidisha spidi yakiwa barabarani (Tochi), na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na Jeshi la polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani katika magari ya abiria nchini.

Makamu wa Rais amefurahishwa na mkakati wa Serikali wauandaaji wa mfumo mpya na wa kisasa wakuweka kamera zitakazorekodi makosa ya usalama barabarani yanayofanywa na madereva nchini.

Ametoa rai kwa Askari wa Usalama Barabarani kutotumia kigezo cha kupiga Tochi kwa kuwaonea, kuwanyanyasa madereva na kudai rushwa kwani vitendo havikubaliki kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo.

“Taswira tunayoitaka ni kuwa wananchi wawaone askari kama walinzi wa malizao na maisha yao na sivinginevyo”, amesisitiza Makamu wa Rais.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amelitka Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na wadau wake kuhakikisha wanabadilisha mbinu za namna ya kukabiliana na tatizo la ajali nchini nakuongeza nguvu katika kudhibiti mwendokasi, ulevi kwa madereva, kutovaa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda, kutofunga mkanda kwa baadhi ya abiria na ukosefu wa vifaa vya kuwalinda watoto wadogo wakiwa kwenye gari.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba (Mb), amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wataboresha na kuunda mbinu mbalimbali ilikudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

Amewataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupunguza ajali za Barabarani na kuwasisitiza madereva kuzingatia sheria za usalama Barabarani kwa nihatua kali zitachukuliwa kwa yeyote anayekiuka sheria hizo.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Barazahilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa (Mb), amesema kuwa Baraza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali ilikudhibiti ajali za barabarani kama utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya Habari kama Televisheni na Redio pamoja na uandaaji wa viperushi na majarida.

Maadhimisho ya Wiki yanenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa yaliyobeba kauli mbiu “Zuia ajali, Tii Sheria – Okoa maisha”, kwa mwaka huu yameadhimishwa mkoani Kilimanjaro amabapo yameshirikisha wadau mbalimbali wa usalama nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.