News

Wataalam wa TANROADS kurejesha mawasiliano Dar es Salaam-Lindi-Mhe Bashungwa

Wataalam wa TANROADS kurejesha mawasiliano Dar es Salaam-Lindi-Mhe Bashungwa

Lindi

25 Machi, 2024

Timu ya wataalamu kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), wanaendelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo la Somanga - Mtama kilometa 220 kutoka Mkoani Lindi kutokana na daraja linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa.

 

Akitoa taarifa leo tarehe 25 Machi 2024 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara katika eneo hilo.

 

“Timu za TANROADS kutoka Mikoa ya Lindi na Pwani zimeungana kuongeza nguvu ili kabla ya mchana safari ziweze kuendelea. Tunawapa pole wasafiri wote kwa changamoto iliyojitokeza”, ameeleza Waziri Bashungwa.

 

Kwa upande wa Mameneja wa TANROADS wa Mikoa ya Lindi na Pwani Mhandisi Emil Zengo na Mhandisi Baraka J. Mwambage wamesema wanafanya kila jitihada haraka, ili kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo ili Wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.