News

PAC YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA BRT III

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wameishauri Serikali kupitia kuangalia uwezekano wa kufanya maboresha katika eneo la daraja la Mfugale TAZARA kwenye makutano ya barabara ili kuondokana na msongamano mkubwa wa magari pindi mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapo kamilika.

Ushauri huo umetolewa leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam, Wakati Kamati hiyo ikiongozwa na Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka kufanya ziara ya kutembelea miradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi (BRT) Jijini Dar es Salaam Awamu ya Tatu.

Amesema wamewashauri waangalie wanatatua vipi tatizo hilo ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza pindi mradi huo utakapokamilika na kuanza kutumika.

Aidha amesema katika eneo lingine ambalo waliangalie ni pamoja na sehemu ya kujenga karakana ya BRT III imekuwa na matatizo mengi, wamekuwa wakipata eneo na kuanza shughuli zao na kuondolewa kwa sababu zisizo za msingi na kufanya kutafuta eneo lingine wakati fedha zimeshatumika katika uandaaji wa karakana eneo hilo.

Amesema miradi inapoanza lazima ipangwe vizuri ili kuoondokana na changamoto ambazo mwisho inaleta ghara,a ya kulipa fedha nyingi pasipo sababu na miradi inashindwa kuendelea bila sababu maalumu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mpaka sasa mkandarasi yupo kwenye asilimia 5% na alikuwa anatakiwa kuwa katika asilimia 15% hivyo mkandarasi huyo ameahidi kuhakikisha anaziba gepu la asilimia hizo kwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana pamoja na kuongeza wafanyakazi.

Pamoja na hayo ameipongeza kamati kwa kuwasaidia kuwapa maelekezo mbalimbali mazuri ambayo yanawasaidia katika utekelezaji.

"Maelekezo ambayo yametolewa na kamati tumeyachukua ambapo tutaenda kuyatekeleza ikiwemo utaratibu wa kupunguza msongamano kwenye daraja la Mfugale pale TAZARA". Amesema.