News

BARABARA YA LUSAHUNGA HADI RUSUMO MKOANI KAGERA KUFUNGUA ZAIDI FURSA ZA KIUCHUMI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi wanaoishi kuzunguka mradi wa Barabara ya Lusahunga – Rusumo Mkoani Kagera kutojihusisha na uhalifu wa vifaa ambavyo vitatumika katika ujenzi huo.

Akizungumza katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Lusahunga – Rusumo yenye urefu wa kilometa 92, Profesa Mbarawa amesema utunzaji huo wa vifaa utasaidia kulinda thamani halisi ya mradi lakini pia kukamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Amesema Barabara hiyo itajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ya nchini China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 153 na Milioni 563, bila kujumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya Shilingi Bilioni 27 na Milioni 641 Laki 5 na elfu Tisa, mia saba arobaini na tatu nukta nane nane.Profesa Mbarawa amesema mradi huo unatekelezwa kwa muda wa Miezi 24.

Ameongeza kuwa katika Mkoa huo ipo miradi mingine Kumi na Tisa ambayo ipo katika hatua mbalimbali ikiwemo Barabara ya Bugene hadi Burigi Chato National Park (km 60) pamoja na Daraja la Kitengule lenye urefu wa mita 140 yenye barabara za maungio zenye urefu wa km 18 ambapo kazi imefikia asilimia 99.

Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila akaeleza sababu za kuchelewa kwa mradi huo ambao Zabuni za ujenzi wa barabara hiyo zilitangazwa tarehe 9 Novemba, 2020 na kufunguliwa tarehe 9 Machi, 2021 na kusema kuwa ilitokana na Wazabuni kushindwa kukidhi matakwa ya mazingira, hivyo Wakala kulazimika kupoteza muda mrefu kupata taarifa zaidi kutoka kwa Wazabuni.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Lusahunga – Rusumo unatekelezwa kwa kugharamiwa na Benki Dunia, kupitia program ya Tanzania
Transport Integration Project (TanTIP).