Directorates

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

1. Muhtasari

Ukaguzi wa ndani ni kitengo huru cha tathmini ya kazi kilichoundwa  ndani ya Wakala  kuchunguza na kutathmini shughuli zake kama huduma kwa Wakala. Lengo la ukaguzi wa ndani ni kusaidia Wakala kutekeleza majukumu yake kwa uhodari na ufanisi. Lengo la ukaguzi ni pamoja na kutathmini na kuboresha ufanisi wa usimamizi, udhibiti taratibu wa utawala kwa gharama nafuu. Kwa ujumla, jukumu la Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni kumsaidia Mtendaji Mkuu katika kusimamia mifumo ya udhibiti wa ndani, usimamizi na uongozi ndani ya Wakala.

Utawala

Ukaguzi wa ndani inalenga katika kuongoza TANROADS katika kuwa na utawala bora na kupambana na rushwa katika Wakala. Kitengo huki kinatathmini mchakato wa utawala kwa lengo la kufanya maboresho muhimu ili kuhakikisha kuwa:

i) Thamani na malengo vinaundwa, vinawasilishwa katika Wakala  na kuhifadhiwa;
ii) Utimizaji wa malengo unafuatiliwa;
iii) Uwajibikaji na uwazi ni unahakikishwa;
iv) Kuna uadilifu sahihi ;
v) Uendeshaji  unazingatia sheria muhimu, kanuni na taratibu;
vi) Kila idara ndani ya Wakala inafanya mambo yake kitaaluma na kimaadili; na
vii) Wakala inadumisha ufanisi katika udhibiti wa ndani ili kuzuia migongano ya wafanyakazi kimaslahi, utovu wa nidhamu, au udanganyifu.


2. Taarifa

Kitengo hiki inaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani  ambaye anaripoti kwa Mtendaji Mkuu. Kitengo kinafanya kazi zake kwa mashauriano na Kamati ya Ukaguzi ya wakala, Usimamizi , na mara kwa mara kushirikiana na wakala  nyingine maalumu za utawala.